Wanaume wanaoripoti kunyanyaswa waongezeka Katavi

By Neema Hussein , Nipashe Jumapili
Published at 02:58 PM Jan 28 2024
Danda la dawati la jinsia lililopo katika maonesho ya wiki ya sheria mkoani Katavi.
Neema Hussein
Danda la dawati la jinsia lililopo katika maonesho ya wiki ya sheria mkoani Katavi.

IMEDAIWA kuwa wanaume wengi kwasasa katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi hutoa taarifa za ukatili wanaofanyiwa ikilinganishwa na hapo awali.

 

Hayo yamesemwa na Hawa Senga kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Manispaa ya Mpanda, wakati akieleza kazi wanazofanya katika banda lao kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Emily Bugoma amesema Jeshi hilo lipo kwa mujibu wa sheria na linapokea mtu yeyote ambaye mahakama imeamuru aende gerezani.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph amewasisitiza wananchi kuitumia wiki ya sheria kufahamu sheria ambazo zinawalinda na kuwapa haki huku Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi Gway Sumaye akidai kwa sasa Mahakama wapo kwenye matumizi ya tehema hivyo nivizuri wananchi kufika katika banda lao kuona matumizi hayo na kutatuliwa changamoto zao.