Israel yadai kumuua Kiongozi wa kundi la Islamic Jihad

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:23 PM May 05 2024
Moshi ukifuka baada ya shambulio la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams karibu na mji wa Tulkarem katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel: 20.04.2024
Picha: Majdi Mohammed/AP Photo/picture alliance
Moshi ukifuka baada ya shambulio la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams karibu na mji wa Tulkarem katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel: 20.04.2024

KIONGOZI wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Islamic Jihad ameuawa katika shambulizi la anga kusini mwa Gaza.

Hayo yameelezwa na Jeshi la Ulinzi la Israel IDF ambalo limesema kwamba Aiman Zaarab alikuwa mmoja wa makamanda wa kundi hilo huko Rafah na kuwa alihusika katika shambulio la Oktoba 7. Wanamgambo wengine wawili wa kundi hilo wameuawa pia katika shambulio hilo.

Wiki hii Israel iliifahamisha Marekani kuhusu mpango wa kuwahamisha raia wa Kipalestina kabla ya uwezekano wa kuanzisha operesheni ya kijeshi huko Rafah katika dhamira ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas. Watu wengine watano wameripotiwa kuuawa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel.

DW