Rais Ruto atoa ya moyoni kuhusu Lowassa

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 04:12 PM Feb 11 2024
Rais Willam Ruto.
PICHA :Na Mtandao
Rais Willam Ruto.

RAIS wa Kenya, William Ruto ametuma salamu za pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa aliyefariki dunia jana, Februari 10, 2024.

Lowassa alikuwa kiongozi anayeheshimika na mpenda maendeleo" ameandika Rais Willam Ruto.

Kupitia ukurasa wa X, Ruto ameandika, “Lowassa alikuwa kiongozi anayeheshimika na mpenda maendeleo Alifanya kazi kwa manufaa makubwa ya wananchi wa Tanzania na ukanda wa Afrika ya Mashariki, tunaheshimu maisha aliyoyaishi, kazi yake na urithi aliouacha nyuma.

“Mungu awape nguvu familia, Rais Samia Suluhu Hassan na watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Buriani Ndugu Lowassa,” ameandika Rais Ruto.