Senegal wapiga kura kuchagua Rais mpya leo

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:22 PM Mar 24 2024
Raia wa Senegal wakiwa tayari kupiga kura.
PICHA: SENEGAL NEWS
Raia wa Senegal wakiwa tayari kupiga kura.

WATU milioni 7.3 nchini Senegal wanatarajiwa kupiga kura leo, ili kuamua kati ya wagombea 17 ambao bado wako kwenye kinyang’anyiro cha kumrithi Macky Sall, aliyeongoza nchi hiyo tangu mwaka 2012, na amezuiwa kuwania tena baada ya kufikisha kikomo katika uongozi huo.

Awali uchaguzi huo wa urais uliopangwa kufanyika Februari 25, na uliahirishwa kufuatia mzozo mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Kuna wagombea 17 ambao wanaenelea kushiriki kinyang’anyiro hiki cha urais kumrithi Macky Sall ambao ni Amadou Ba, Boubacar Camara, Aliou Mamadou Dia, Mamadou Lamine Diallo, El Hadji Mamadou Diao, Mahammed Boun Abdallah Dionne, Déthié Fall, Papa Djibril Fall, Bassirou Diomaye Faye, El Hadji Malick Gakou, Serigne Mboup, Daouda Ndiaye, Aly Ngouille Ndiaye, Anta Babacar Ngom, Khalifa Sall, Thierno Alassane Sall na Idrissa Seck.

Vituo 16,440 vya kupigia kura vimefunguliwa leo Machi 24, pamoja na vituo 807 kwa nje ya nchi. Matokeo ya muda ya duru hii ya kwanza yatatangazwa kabla ya Ijumaa Machi 29.

Katika tukio la duru ya pili, hii itaandaliwa Jumapili ya pili baada ya Baraza la Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza.