Waislam wahimizwa kuipenda Quran

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 03:29 PM Apr 28 2024
Mkuu wa Tawi la Chuo Kikuu cha Al Mustapha Tanzania, Aci Taghavi.
Picha: Halfani Chusi
Mkuu wa Tawi la Chuo Kikuu cha Al Mustapha Tanzania, Aci Taghavi.

Mkuu wa Tawi la Chuo Kikuu cha Al Mustapha Tanzania, Ali Taghavi amewataka waislam duniani kuipenda quraan akisistiza ni kitabua pekee ambacho waumini wote wamekubaliana kukitumia na kimetoka kwa Mungu kupitia Mtume Muhammadi.

Ali Taghavi ameyasema hayo leo jijin Dar es Salaam Katika kongamano la Kimataifa la 29 ambapo ni mara ya pili kwa kongamano hilo kufanyika Dar es Salaam.

Amesema Katika kongamano Hilo watagawa zawadi kwa washindi waliopatikana kutokana na kuhifadhi na kusoma quraani vizuri. 

"Leo tutawapa zawadi washindi na kuwaongeza lengo ni kuwaweka watu karibu na kuipenda quran" amesema