Director Khalfani Afariki dunia

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 11:07 AM May 05 2024
Director Khalfani Khalmandro.
picha: maktaba
Director Khalfani Khalmandro.

MUONGOZAJI wa video za muziki nchini Tanzania, Director Khalfani Khalmandro, amefariki Dunia leo asubuhi Mei 5, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zilieleza kuwa Khalfani alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taasisi ya mifupa MOI akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililopelekea changamoto ya kupooza upande wake wa kulia wa mwili.

Enzi za Uhai wake alijipatia umaarufu kwa kuongoza Video za Wasanii kama Aslay, NavyKenzo, Christian Bella, Baby Madaha, Chinbees, Shilole na Linah.