Bangladesh yakabiliwa na joto kali

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:14 PM Apr 28 2024
Bangladesh yakabiliwa na joto kali.
PICHA: MAKTABA
Bangladesh yakabiliwa na joto kali.

MAMLAKA nchini Bangladesh zimetoa tahadhari nyingine ya joto kali kwa siku tatu kuanzia leo Jumapili, miaka 75 iliyopita taifa hilo la kusini mwa Asia limewahi kukabiliwa na wimbi hilo la joto kali .

Siku ya Ijumaa, nchi hiyo iliripoti kiwango cha juu cha nyuzi joto 42.7 katika kipimo cha Celcius katika wilaya ya kusini magharibi ya Chuadanga.

Joto kali limeilazimu serikali kufunga shule kwa wiki nzima, huku hospitali zikijiandaa kupokea idadi kubwa ya wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi yatokanayo na joto kali, ikiwemo upungufu wa maji mwilini, uchovu na matatizo ya kupumua.

Wimbi la joto kali limedumu kwa siku 29 kufikia leo Jumapili, ikiwa ni kipindi kirefu tangu mamlaka nchimo humo zilipoanza kutunza rekodi za hali ya hewa.