Ghorofa laporomoka na kuuwa watu watano

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:14 PM May 07 2024
Jengo la ghorofa laporomoka Afrika Kusini.
Picha: Tarekuzzaman
Jengo la ghorofa laporomoka Afrika Kusini.

WATU watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa kwa kunasa chini ya vifusi baada ya jengo kubwa la ghorofa lililokuwa bado linajengwa kuporomoka katika Mji wa George huko nchini Afrika Kusini.

Mamlaka nchini humo zimesema kuwa watu 24 wameokolewa lakini wengine wapatao 51 bado hawajapatikana. Uongozi wa jiji hilo la pwani umesema kuwa mafundi 75 walikuwa katika jengo hilo wakati likipoporomoka jana alasiri.

Aidha, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametolea salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza jamaa zao na kuamuru kufanyike uchunguzi wa kina.

DW imerpoti kuwa, Mji wa George wenye wakazi 160,000 unapatikana katika eneo linalopendwa mno na watalii katika ukanda wa pwani ya kusini mwa nchi hiyo.