Mafuriko yakwamisha safari Dubai Airport

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:56 PM Apr 18 2024
Uwanja wa ndege wa Dubai.
PICHA: MAKTABA
Uwanja wa ndege wa Dubai.

MVUA kubwa ambayo inaendelea kunyesha Dubai na kusababisha mafuriko makubwa imeendelea kuleta athari mbalimbali ikiwemo kukwamisha safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Dubai ambao ni uwanja wa pili kwa shughuli nyingi zaidi Duniani.

Kutokana na picha na video zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ndege zimeonekana zikielea juu ya maji, huku Uongozi wa Dubai Airport ukitoa tahadhari na kuwashauri baadhi ya abiria kutofika kutokana na maeneo mengi kusombwa na maji.

Jana Jumatano safari 300 za ndege kwenda na kutoka nchini Dubai zilighairishwa kwa mujibu wa data za Flight Aware na abiria wengi walichelewa safari zao, Shirika Kuu la Ndege la Kimataifa lenye Makao yake makuu Dubai, lilisimamisha uingiaji kwa abiria hadi leo Alhamisi.

Dubai Airport imehudumia zaidi ya abiria milioni 80 mwaka jana na ni Airport ya pili kwa kubeba watu wengi Duniani baada ya Atlanta ya Nchini Marekani, Mamlaka za Dubai zimetahadharisha kuwa mvua nyingi zaidi za radi zinatarajiwa zikiambatana na upepo mkali, huku maeneo mengi ya mabondeni yakiwa bado chini ya maji.