Wafanyakazi wa Kenya Airways waliozuiwa DRC waachiwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:13 PM May 07 2024
Kenya Airways.
PICHA: MAKTABA
Kenya Airways.

OFISA Mwadamizi wa Wizara ta Mambo ya Nje nchini Kenya, amethibitisha kuachiliwa huru kwa wafanyakazi wa Shirika la Ndege nchini humo waliokuwa wamekamatwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kitengo cha ujasusi wa kijeshi cha DRC kilizuia wafanyakazi wawili wa shirika hilo Aprili 19, mwaka huu kwa madai ya kukosa nyaraka za forodha kwenye baadhi ya mizigo ya thamani.

Wawili hao walizuiwa licha ya agizo la Mahakama kutaka waachiliwe. Mmoja wa wafanyakazi hao ni raia wa Kenya na mwingine raia wa DRC.