Balozi Iran nchini asisitiza amani

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 01:06 PM Apr 28 2024
Balozi wa Iran nchini Hussein Alvandi, (Wa kwanza kushoto) akiwa Katika Kongamano la 29 la Ali Mustapha International University.
Picha: Halfani Chusi
Balozi wa Iran nchini Hussein Alvandi, (Wa kwanza kushoto) akiwa Katika Kongamano la 29 la Ali Mustapha International University.

Balozi wa Iran nchini Hussein Alvandi, amesema Quran na utamaduni ni nyenzo kubwa ya Kudumisha ushirikiano kati yao na Tanzania.

Balozi huyo ameyasema hayo leo jijin Dar es Salaam, Katika Kongamano la 29 la Ali Mustapha International University akisistiza Quran ndio kitabu pekee ambacho kimetoka kwa mwenyezi Mungu kupitia Mtume Mohammed na kwamba kikitumika vizuri kinaweza kuleta amani.

"Pia kitasaidia kukuza uhusiano sehemu nyingine ambayo inayoweza kuwa chachu ni kukuza utamaduni na tunaweza kushirikiana kati ya Tanzania na Iran.

"Ukiiangalia historia ya Tanzania miaka ya nyuma iliyopita walikuwapo watu wanaitwa washirazi na hao mpaka leo wameacha historia katika nchi yetu kwahiyo kati ya Iran na Tanzania tunaweza kushirikiana kukuza amani" amesema