Dk. Nchimbi: Tupinge rushwa kwa vitendo

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 07:50 PM Apr 18 2024


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.
Picha: Halfani Chusi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi , amewataka Watanzania wote kujituma na kufanya kazi kwa bidii huku akionya kujihusisha na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa.

"Endeleeni kuchapa kazi kwa bidii , kufanya kazi zitakazokuingiza kipato kihalali lakini jiepusheni na rushwa kwakuwa siku zote ndio adui wa haki, kuchapa kazi ni kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuwataka Watanzania wote kufanya kazi na ndipo tutazidi kulijenga taifa letu na kuimarika kiuchumi"

Vilvile, Balozi Balozi Nchimbi amesema Jeshi la CCM (Viogozi wa kitaifa) wataendelea kuhakikisha wanaisimamia serikali ipasavyo katika kutimiza wajibu wao na kutekeleza ilnai ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.

Balozi  Nchimbi ameyasema hayo wakati alipopokelewa na vongozi, wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.

Katibu wa Uenezi Itikadi na Mafunzo CCM Taifa,  Amos Makalla amesema serikali imetoa Sh bilioni 138 kwaajili ya kujenga barabara ya njia nne kutoka Nsalaga kwenda Ifisi.

"Ili kuonyesha kwamba serikali inajali wananchi wake tayari Barabara imeanza kujengwa kwaajili ya kupunguza foleni, laini upo mpango wa kujenga barabara kama hizo kutoka igawa mpaka tunduma na wakati wowote mkandarasi ataanza kazi" alisema Makala huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho

Vilevile amewataka wafuasi wa chama hicho kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan Katika uchaguzi wa mwakani  akisistiza amefanya mambo makubwa Katika mkoa wa Mbeya.

Makalla amegusia lengo la ziara hiyo kuwa imelenga mambo manne ikiwamo kuangalia uhai wa chama, ilani ya uchaguzi, maandalizi ya uchaguzi na utatuzi wa kero.

Amesema tangu walipoanza ziara hiyo Katika mkoa wa Katavi wamefanikiwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi 114 kwa njia aliyoiita ya kisayansi.

Katibu wa Oganaizesheni CCM Taifa Issa Gavu, alisema ushindi kwao ni jambo la lazima na kwamba wamejiandaa na wako tayari kushinda na kushika dora. 

Amesema upendo na mshikamano ni mbinu ya kushinda Katika uchaguzi ujao huku akiwataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha Katika  daftari la kudumu la wapiga kura. 

"Ninaagiza wafuasi wa chama chetu kuchagua viongozi wanaoweza kutatua shida za watu, bila shaka yoyote  kwa sababu ndani  ya CCM ndiko kwenye viongozi wazuri" amesema Gavu.