Dk. Yonazi afanya mazungumzo na TECDEN

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:09 PM May 07 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Merina  Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo.
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dk. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Jijini Dodoma.

Dk. Yonazi amekutana na uongozi huo leo Mei 7, 2024 ambapo wamejadili kuhusu kazi za Taasisi hiyo ikiwemo ya uratibu wa Mashirika na Wadau wasio wa Kiserikali katika masuala mazima ya malezi, makuzi ya awali ya watoto wadogo kuanzia umri 0 hadi miaka minane.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi hiyo ili kuendelea kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa katika sula la makuzi kwa watoto.