Wajikusanya upya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji chao

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 02:35 PM Apr 30 2024
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakiwa na vitabu vinavyoelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 walivyokabidhiwa na mbunge huyo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakiwa na vitabu vinavyoelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 walivyokabidhiwa na mbunge huyo.

WAKAZI wa Kijiji cha Kataryo kilichopo Kata ya Tegeruka Musoma Vijijini, wamekubaliana na kuongeza kasi ya ujenzi zahanati ya kijiji ili ianze kutoa huduma.

Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vitatu vinaunda Kata hiyo, vikiwamo vya Mayani na Tegeruka.
Hata hivyo, hakina zahanati, kitendo kinachosababisha wakazi wake kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita saba kwenda kupata huduma za afya katika zahanati ya Kijiji jirani cha Mayani.

Wakazi wa Kataryo walia za ujenzi wa zahanati yao Julai mwaka 2023, lakini bado ujenzi huo unasuasua hadi sasa.

Mbunge wa  Musoma, Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amesema, Aprili 4 mwaka huu alikaribishwa kufanya harambee ya kuchangia ujenzi huo, ambapo wakazi wa vitongoji sita vya kijiji hicho walikubaliana kuchangia vifaa vya ujenzi kulingana na wingi wa kaya za kila kitongoji.

"Michango ya awali ilikuwa kati ya shilingi 5,000 hadi 7,000 kwa kila kaya, saruji kutoka kwa mbunge ilikuwa ni mifuko 200 na nyingine  kutoka kwa diwani, Alpha Mashauri ilikuwa mifuko 50," amesema Prof. Muhongo

Jengo la zahanati ya Kijiji cha Kataryo ambalo wananchi wamemua kujipanga upya ili kukamiliaha ujenzi wake.
Amesema, katika  harambee hiyo,  wanakijiji walichangia mifuko 26 ya saruji na shilingi 600,000, ambalo pia wanaomba wadau wa maendeleo kuchangia ujenzi huo.

"Akaunti ya kijiji ya kuweka michango hiyo ni ni Benki ya NMB Na 30302300302, jina ni Kijiji cha Kataryo," amesema.

Kuhusu huduma za afya jimboni humo, amesema kuna vijiji 68 na kata 21, hospitali moja yenye hadhi ya wilaya ya wilaya.

"Kuna vituo sita vya afya na zahanati 25 za serikali 25 za serikali na nne za binafsi, huku nyingine 16 zikiendelea kujengwa ikiwamo ya Kataryo," amesema.