Dk.Mwigulu ampongeza GSM mafanikio ya Yanga, ataka ajengewe mnara

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:24 PM Jun 13 2024
news
Picha: Yanga SC
Ghalib Said Mohamed (GSM)

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni Jijini Dodoma leo June 13,2024 amempongeza GSM kwa mafanikio aliyoyafanya kwenye klabu ya Yanga SC.

“Kwa umaalum kabisa nimpongeze GSM kwa uwekezaji mzuri alioufanya ambao umebadilisha kabisa taswira na uwezo wa kiuchezaji wa Timu ya Yanga, mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mzuri uliofanywa na GSM ( Ghalib Said Mohamed), GSM wewe ni Mwamba, ujengewe Sanamu/Mnara pale Makao Makuu ya Yanga”

“Nitoe pongezi kwa Menejimenti bora ya Timu chini ya Injinia Hersi Saidi kwa kuiongoza vyema timu ya Wananchi Yanga na kuipeperusha bendera ya Nchi yetu katika medani za kimataifa, kama tunavyofahamu Tanzania iliingiza timu bili katika hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya soka Nchini, pamoja na kwamba wenzetu Simba walipigwa ndani nje katika hatua hiyo lakini ni sehemu ya kujifunza na kujipanga upya”

“Kipekee, niipongeze Timu ya Yanga kwa kuitoa jasho timu ya Mamelodi Sundowns, nina uhakika ile ya mechi ya mwisho kule Afrika Kusini, wale Wachezaji wa Mamelodi Sundowns walilala na viatu kufuatia kitu kizito walichokumbana nacho uwanjani” ——— asema Dk. Mwigulu Nchemba akisoma bajeti kuu ya Serikali 2024/2025.

1

“Mafanikio ya Yanga na Klabu nyingine yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na hamasa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ambapo amekuwa akitoa shilingi milioni tano kwa kila goli linalofungwa katika hatua ya makundi na shilingi milioni kumi kuanzia hatua ya robo fainali. Hivyo, kwa namna ya pekee naomba nitoe pongezi kwa Mama yetu kwa ubunifu huo ambao umeliletea Taifa letu sifa na heshima 164 kubwa katika nyanja ya michezo”

“Rai yangu kuwa tuendelee kuhamasisha michezo mingine ili Nchi yetu iweze kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na hatimaye kurudi na tuzo au makombe, aidha napenda kutumia fursa hii kuipongeza Timu ya YANGA kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya kandanda nchini kwa mara ya tatu mfululizo na Kombe la Shirikisho”

“Yanga ni Wafalme wa soka la Tanzania, natamani kumshauri Gavana wa Benki kuu kuweka nembo ya klabu ya Yanga kwenye noti ya shilingi 100 kuyaenzi mafanikio haya” ——— Dk. Mwigulu Nchemba