‘Mlango kwa mlango’ elimu ya mlipa kodi Katavi

By Neema Hussein , Nipashe
Published at 07:30 PM Apr 30 2024
Maofisa wa TRA wakitoa elimu ya mlipa kodi ‘malango kwa mlango’.
PICHA: NEEMA HUSSEIN
Maofisa wa TRA wakitoa elimu ya mlipa kodi ‘malango kwa mlango’.

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewataka maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanatumia kampeni ya mlango kwa mlango kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara huku akiwasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ndani na nje ya mkoa wa Katavi.

Mrindoko ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo kwa maafisa wa TRA kutoka makao makuu ambao wametiatimu Katavi wakishirikiana na maafisa wa TRA mkoa wa Katavi kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara ikiwa nipamaoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili huku Meneja TRA mkoa wa Katavi Nicholaus Migera akidai hali ya utoaji wa risiti bado hairidhishi.

Nae Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Katavi Amani Mahela amewaomba maafisa wa TRA kutotanguliza adhabu badala yake watangulize ubinadam ikiwa nipamoja na kuwalea wafanyabiashara wadogo ili waweze kukua kiuchumi huku baadhi ya wafanyabiashara wakiomba elimu kwa  mlipa kodi iwe endelevu ili watoa huduma kwa ufanisi.

Mkoa wa Katavi unajumla ya wafanyabiashara 12,000 ambao tayari wamesajiliwa.