KIONGOZI wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Islamic Jihad ameuawa katika shambulizi la anga kusini mwa Gaza.
Hayo yameelezwa na Jeshi la Ulinzi la Israel IDF ambalo limesema kwamba Aiman Zaarab alikuwa mmoja wa makamanda wa kundi hilo huko Rafah na kuwa alihusika katika shambulio la Oktoba 7. Wanamgambo wengine wawili wa kundi hilo wameuawa pia katika shambulio hilo.
Wiki hii Israel iliifahamisha Marekani kuhusu mpango wa kuwahamisha raia wa Kipalestina kabla ya uwezekano wa kuanzisha operesheni ya kijeshi huko Rafah katika dhamira ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas. Watu wengine watano wameripotiwa kuuawa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
DW
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED