Polisi Uturuki yakamata waandamanaji 200

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:59 AM May 02 2024
Maafisa wa polisi wa Uturuki wakikabiliana na waandamanaji wanaojaribu kuandamana kuelekea uweanja wa Taksi.
Picha: KEMAL ASLAN/AFP
Maafisa wa polisi wa Uturuki wakikabiliana na waandamanaji wanaojaribu kuandamana kuelekea uweanja wa Taksi.

POLISI nchini Uturuki, wamewatia mbaroni waandamanaji 200 waliokuwa wakiandamana baada ya mamalaka kupiga marufuku mikusanyiko ya kuadhimisha Mei Mosi iliyopangwa kufanyika katika uwanja wa kihistoria wa Taifa hilo wa Taksim huko mjini Istanbul.

Waandishi wa AFP wameripoti kuwa, polisi walikabiliana na waandamanaji karibu na ukumbi wa jiji katika wilaya ya Sarachane, wakifyatua mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwazuia waandamanaji kuvunja vizuizi.

Kupitia ukurasa wake wa X, Waziri wa mambo ya ndani, Ali Yerlikaya, ameandika “Watu 210 wamekamatwa Istanbul kwa kutotii onyo lao na kuwashambulia polisi siku ya Mei Mosi,”

Zaidi ya polisi 40,000 walisambazwa kote Istanbul, wakizuia mitaa midogo ya pembeni kwa vizuizi vya chuma katika jaribio la kuzuia waandamanaji kukusanyika.