Kiongozi Mbio za Mwenge atoa rai wawekezaji kuzingatia sheria

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 05:54 PM May 04 2024
Mwenge wa Uhuru 2024.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwenge wa Uhuru 2024.

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava ametoa rai kwa wawekezaji kuzingatia Sheria za kazi na kuepuka vitendo vya unyanyasaji kwa wafanyakazi.

Mzava pia amewataka wananchi walioajiriwa kuwalinda Imani waliyopewa kwa kuepuka matendo ambayo yanaweza kuharibu taswira ya kiwanda .

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ametoa rai hiyo Mei 4 alipokuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Dunda Wilaya ya Mkuranga Mwenge huo ulipopita kuweka jiwe la Msingi kiwanda cha kubangua korosho cha Tan-Ko Mirae green Co LTD.

" Rai ya Mwenge wa Uhuru kila kitu kifuate utaratibu unavyotaka zingatia utu wa watu ustawi wa wafanyakazi uangaliwe malengo ya Mwenge yazingatiwe ikiwa ni pamoja na kuzingatia utu wa mtu" amesisitiza.

Amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na pia Taasisi wezeshi zimezingatia hayo hivyo wawekezaji na wafahyakazi nao wa atakuwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo.

Amesisitiza wawekezaji wa kiwanda hicho kuwa makini kepuka vitendo vya unyanyasaji, na kwamba endapo mfanyakazi akienda kinyume taratibu za kisheria zinatakiwa zifuatwe badala ya kumpiga na kumnyanyasa mfanyakazi.

Katika kiwanda hicho cha kubangua korosho makadirio ya mapato kwa kipindi cha miaka mitatu ya kwanza kinatarajiwa kufikia Biln 12.9 na kwamba tani 9,600 za korosho mbichi zitabanguliwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema wamiliki wa viwanda wanatakiwa kufanya kazi na vijana kwa staha Ili kila mmoja atimize malengo aliyojiwekea.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Kisarawe, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri amesema Mwenge huo utakimbizwa km 85 utakagua, kuzindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi 13 yenye thamani ya sh.Biln 10.2

Mwenye wa Uhuru 2024 umepitia pia  mradi wa  Uhifadhi wa  mazingira ambao unasimamiwa na  Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) , mradi wa vijana wanqojishughilisha na utengenezaji wa samani, mradi wa lishe, Barabara km 0.48 kiwango cha lami, ujenzi na ukarabati Hospitali ya Wiilaya, Malaria na Ukimwi.