KUELEKEA MEI MOSI 2024: THTU yabainisha maeneo mwiba kwa wafanyakazi

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 05:10 PM Apr 24 2024
Mwenyekiti wa THTU Taifa, Dk.Paul Loisulie.
Picha: Paul Mabeja
Mwenyekiti wa THTU Taifa, Dk.Paul Loisulie.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU), kimetaja maeneo ambayo yamekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyakazi kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na ukokotoaji mafao, hali inayopunguza morali ya kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa , Mwenyekiti wa THTU Taifa, Dk.Paul Loisulie, amesema kwa siku za karibuni, kumetokea changamoto kadhaa kuhusu sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa mafao katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania.

“THTU imebaini changamoto zinazoathiri haki ya mfanyakazi kupata stahiki husika pindi anapostaafu, kama inavyobainishwa hapa chini,”amesema.

Amesema kikokotoo kinachotumika hakiakisi hali halisi ya wanachama na kupendekeza kifanyiwe mabadiliko kwa kuongeza umri baada ya kustaafu kutoka miaka 12.5 hadi 15.5 wanachama wapewe angalau asilimia 50 kama mafao ya mkupuo itumike 1/540 badala ya 1/580.

Kuhusu uhai wa mfuko wa NHIF, amependekeza fedha za mfuko zitumike kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

“Hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu wote waliofanya udanganyifu kwenye matumizi ya fedha za mfuko Kuwe na kifungu katika sheria inayoitaka Bodi ya Mfuko kupata ushauri wa kitaalam kabla ya kuwekeza fedha za mfuko na pia kuwe na mfumo bora wa usimamizi na udhitibi wa vihatarishi,”

1