Marufuku kuvuta sigara hadharani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:37 PM Apr 30 2024
Bunge lakataza kuvuta sigara hadharani.
PICHA: MAKTABA
Bunge lakataza kuvuta sigara hadharani.

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema Bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ambayo imetoa katazo la uvutaji wa sigara hadharani.

Mollel amebainisha hayo Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tumbe, Amour Khamis Mbarouk, aliyeuliza ni lini Serikali italeta sheria ya kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.
 
 Dk. Mollel amewataka wabunge kuwa mabalozi wa udhibiti wa tumbaku katika jamii, ili kusaidia wananchi kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza, huku akisema kuwa sheria pia imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.