Prof. Mbarawa awasilisha vipaumbele vya bajeti Wizara ya Uchukuzi

By Dotto Charles , Nipashe
Published at 09:37 AM May 07 2024
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
PICHA: MAKTABA
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma leo, Mei 6, 2024, ambapo ameliomba Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo ambayo ni zaidi ya shilingi trilioni 2.

Prof. Mbarawa, amesema katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara hiyo itatumia kiasi cha shilingi 2, 729,676,417,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amesema fedha hizo zitatumika katika miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa tayari imeshaanzishwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa, kukarabati reli iliyopo katika MGR, kuendelea kuboresha na kuimarisha Shirika la ndege Tanzania (ATCL) na ukarabati wa meli katika maziwa makuu.