RC Ayoub kugawa mikate kwa wafanyakazi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:54 AM May 05 2024
Chai na mkate.
PICHA: MAKTABA
Chai na mkate.

MKUU wa Mkoa wa kusini Unguja Visiwani Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahamoud, ametangaza kuwapatia Wafanyakazi wa Ofisi hiyo chai ya asubuhi ikiwa na kitafunwa cha mkate wenye siagi kuanzia kesho Jumatatu Mei 06, 2024 ili kupunguza wafanyakazi kuzurura saa za kazi, kuongea na simu mara kwa mara pamoja na kutoka nje kwenda kununua urojo.

RC Ayoubu ameyasema hayo leo wakati akifungua kampeni ya ‘amshaamsha Kusini’ ikiwa na mahususi kwa watumishi wa serikali lengo likiwa ni kutokomeza uchelewaji makazini, kuzurura muda wa kazi na matumizi ya simu vitu ambavyo amesema haridhishwi navyo kwani vinachelewesha maendeleo ya wananchi ambapo amesisitiza kuwa gharama zote za chai na vitafunwa zitakuwa zikitoka kwenye mshahara wake yeye Mkuu wa Mkoa.

“Nitaanza Jumatatu ya tarehe 6 na sitotoa pesa hii kwenye mfuko wa Serikali bali nitatoa kwenye sehemu ya mshahara wangu ili kuleta ufanisi kwenye Ofisi, Watumishi wengi baada ya kupata mshahara siku chache wanakuwa hawana pesa ndio maana wanapata shida ya kuhangaika ya huku na kule” amesema RC Unguja Ayoub Mohammed.