Silaa aagiza wananchi wamilikishwe ardhi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:54 PM Apr 25 2024
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.
PICHA: MAKTABA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewaagiza wataalamu wa idara ya ardhi wilayani hapa Mkoa wa Tanga kuendeleza upimaji, upangaji na umilikishaji ardhi kwa wananchi.

Silaa ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake wilayani hapa baada ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na migogoro ya ardhi na kuzipatia majibu na nyingine kumuachia Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah.

Shughuli hiyo imeambatana na uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi wilayani hapa kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kutatua migogoro ya ardhi.

Silaa, amesema wataalam wa ardhi wasijufungie ofisini  badala yake waende kutekeleza majukumu ya kupima viwanja, kupanga na kumilikisha  wananchi ardhi ili kusitokee migogoro.