Wanachukua misaada ya waathirika wa mafuriko kukiona

By Neema Hussein , Nipashe
Published at 06:08 PM May 02 2024
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko (Kushoto) akigawa misaada mbalimbali kwa waathrika wa mafuriko.
PICHA: NEEMA HUSSEIN
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko (Kushoto) akigawa misaada mbalimbali kwa waathrika wa mafuriko.

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameziagiza kamati za ulinzi na usalama za mkoa na wilaya kuchukua hatua za haraka kwa mtuyeyote atakaebainika kufanya ubadhilifu wa misaada iliyotolewa kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi.

Mrindoko ameyasema hayo wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ambapo amesema serikali ya mkoa wa Katavi haikotayari kuona watu wachache wanafanya hujuma juu ya misaada iliyotolewa.

Akisoma taarifa ya uharibufu uliosababishwa na mafuriko mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika ambae ni Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri hiyo Halima Kitumba amesema jumla ya magari 16 yalikwama huku kaya zaidi ya 1000 zikiathirika.

Kwaupande wao waathirika wa mafuriko waliopatiwa msaada wameishukuru serikali huku wakitoa ushauri wa kuhakikisha wanadhibiti maji ambayo yanaelekea kwenye makazi ya watu.

Msaada uliotolewa unathamani ya shilingi milioni 113.3 ambao umegawanywa katika halmashauri zote zilizokubwa na mafuriko mkoani Katavi kwalengo la kugawa kwa wahanga katika vijiji mbalimbali vya halmashauri hizo.