Watoto watatu wa familia moja wafariki kwa kuangukiwa na nyumba

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:58 AM Apr 26 2024
Watu wakiwa kwenye nyumba ambayo imeanguka na kusababisha vifo vya watoto watatu wa familia moja.
Picha: Mpigapicha Wetu
Watu wakiwa kwenye nyumba ambayo imeanguka na kusababisha vifo vya watoto watatu wa familia moja.

Watoto watatu wa familia moja mkoani Shinyanga wamefariki dunia usiku wa kumakia leo, Ijumaa Aprili 26,2024 baada ya kuangukiwa na nyumba walimo kuwa wamelala.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Miembeni B, Kata ya Mwantini, Masai Senema, inasema kuwa Watoto hao ni wa familia ya Ngasa Mataluma.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea baada ya nyumba hiyo waliyokuwa wamelala na mama yao Kashinje Nchembi kuanguka kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.