WVA,WOAH washirikiana kutoa elimu ya wanyama kuhusu magonjwa ambukizi

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 07:02 PM Apr 29 2024
Baadhi ya wakazi wa  Kilolo mkoani Iringa wakipatiwa huduma ya chanzo mbwa wao.
Picha: Mpigapicha Wetu
Baadhi ya wakazi wa Kilolo mkoani Iringa wakipatiwa huduma ya chanzo mbwa wao.

CHAMA cha Mifugo Duniani (WVA) kwa kushirikiana na Shirika la Afya ya Wanyama (WOAH) imetoa elimu ya wanyama kuhusu magonjwa ambukizi kwa wanafunzi pamoja kutoa huduma za matibabu kwa mifugo kwa wananchi wafugaji katika kufunga maadhimisho ya siku ya wanyama huko Kilolo mkoani Iringa.

Lengo ikiwa ni kudhibiti magonjwa ya  mifugo, kulinda afya ya mifugo, kulinda afya ya jamii, kuhamasisha biashara salama ya mifugo na mazao yake.

Daktari wa mifugo mtafiti  mwandamizi pia Katibu wa Chama Cha Madaktari wa Wanyama Nyanda za Juu kusini Dk.Jofyey Mbata amesema hayo ni maadhimisho ya Pili Kitaifa nchini waliamua kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa ya wanyama kwa ujumla.

Ikiwemo utoaji wa chanjo dhidi wa ugonjwa wa sokota (PPR) kwa mbuzi na kondoo, utoaji chanzo dhidi ya kichaa cha mbwa na paka, kufanya uchunguzi na matibabu ya wanyama katika magonjwa mbalimbali, upasuaji mdogomdogo utoaji kizazi kwa mbwa na paka, utoaji elimu na kuongeza hamasa kuhamasisha uelewa kwa jamii kutambua uwepo wa madaktari wa wanyama Tanzania.

Amesema kuwa, jamii kubwa nchini wamekuwa hawatambui uwepo wa madaktari wa wanyama hali inayofanya kuwepo na shida kubwa ya maambukizi ya magonjwa ya wanyama.

Aidha katika maadhimisho hayo pia walifanikiwa kutembelea shule tatu za msingi na Sekondari zilizopo Manispaa hiyo kuweza kutoa elimu kwa wanafunzi.

Dk. Obed Kihariro Daktari wa mifugo amebainisha kuwa siku ya wanyama duniani ikienda sambamba na utoaji elimu kwa umma  hasa wananchi wafugaji inasaidia kwa kiwango kikubwa  kupata utambuzi wa magonjwa hatarishi kwani kuna magonjwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Hivyo wananchi kupata uelewa na imeonyesha wananchi wengi wamekuwa hawana uelewa kuhusiana na elimu hizo wanafuga mifugo kiholela hali ambayo ni hatari katika jamii.

“Tumewaongezea elimu wafugaji kuhusiana na magonjwa ambukizi na kuwafanyia upasuaji baadhi ya mifugo tuliowakuta na magonjwa ikiwemo kuwapa huduma ya chanjo za minyoo kwa mbwa” amefafanua

Naye Dk.Julius Mahenge amesema matibabu ya minyoo ikiwemo kuwapa elimu ufugaji bora wa mbwa imetolewa bila kuathiri watu wengine chini ya madaktari wa mifugo Tanzania(TVA) na Chuo cha Mifugo na Sayansi ya Tiba (CVMBS) huko SUA.

Amefafanua utoaji huduma hizo za afya ya wanyama zitatolewa bila malipo ili kuleta utambuzi kwa umma wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na matibabu ya kesi za kliniki kwa wanyama wa kufugwa na wanyama na wa kawaida.

Vilevile Kutoa uelewa juu masuala ya afya ya wanyama kwa wamiliki wa uzalishaji wanyama na wanyama kipenzi, uhamishaji wa watoto wa shule za msingi na sekondari juu ya umuhimu wa taaluma ya mifugo ili wahamasike kuendelea na masomo yahusuyo wanyama.