EWURA yanena kuhusu vituo vya mafuta vilivyo karibu na makazi

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 05:30 PM May 02 2024
Mhandisi Mwandamizi wa Mafuta EWURA Kanda ya Magharibi, Ibrahim Kajugusi akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa waandishi.
Mhandisi Mwandamizi wa Mafuta EWURA Kanda ya Magharibi, Ibrahim Kajugusi akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa waandishi.
Mhandisi Mwandamizi wa Mafuta EWURA Kanda ya Magharibi, Ibrahim Kajugusi akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa waandishi.

MAMLAKA ya udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) imetoa ufafanuzi juu ya vitu vya mafuta vilivyojengwa karibu na makazi, ikisema hakuna madhara yoyote yanayoweza kujitokeza kwa sababu vipo umbali wa mita 15 kutoka kwenye makazi na mantaki yake yamechimbiwa chini ya ardhi.

Mhandisi Mwandamizi wa Mafuta EWURA Kanda ya Magharibi, Ibrahim Kajugusi ameyabainisha haya leo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari 30 wa mkoa wa Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uelewa zaidi juu udhibiti wa nishati na maji kwa mlaji ili kutomuathiri.

Amesema, nikweli vituo vingi vya mafuta vinajengwa karibu na wananchi kwa lengo la kusogeza huduma karibu yao na vikijengwa nje ya mji vyote wangelakamika, vinajengwa kwa kuzingatia umbali baina ya wananchi na vituo kwa mitaa 15 na kituo kimoja na kingine kwa umbali wa mita 200 na kuendelea. 

Pia Kajugusi amesema, wameendelea kuweka mazingira na masharti wezesha kwa wafanyabiashara ambao wanataka kujenga vitu vya mafuta vijijiji ili kusogeza huduma na kuondokana na kuuza mafuta ovyo kwenye makazi ya watu ambayo kwasasa yamegeuzwa kuwa sheria za mafuta.

Aidha amesema, mpaka April 30 mwaka huu mpaka sasa wanavitu vya mafuta 464 vilivyojengwa vijijini kwa lengo la kusogeza huduma, na kuwataka wale wanaofanya biashara ya kuuza mafuta ndani kinyemela kuacha mara moja kabla ya kubainika na kuchukuliwa hatua kwani muda wowote wanaweza kuanza msako na kuwabaini. 

Mwandishi wa Habari wa Gazeti hili Neema Sawaka amesema, katika Kata ya Ulowa na maeneo mengine ya Halmashauri ya Ushetu kuna baadhi ya wananchi wanakaa ndani na mafuta zaidi ya lita 500 kwenye pipa na wanayasafirisha kutoka mjini hadi vijijini kwa kutumia magari ya abiria jambo ambalo ni hatari sana. 

Amedai kuwa, miaka kadhaa iliyopita kunafamilia kulitokea janga la moto baada ya mafuta kuripuka na watu kadhaa kupoteza maisha na wamekuwa wakiyauza kupitia kwenye chupa za maji ya kunywa na tena wanayaweka juani bila kufahamu yakipata joto yanaripuka au kupoteza ubora wake.