Vimbunga vyaua wanne Marekani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:34 AM Apr 29 2024
Kimbunga chasababisha uharibifu, Arkansas, Marekani.
Picha: Peter Zay/AA/picture alliance
Kimbunga chasababisha uharibifu, Arkansas, Marekani.

WATU wanne wanadaiwa kufariki dunia kutokana na vimbunga vikali vilivyozuka huko katika Jimbo na Oklahoma nchini Marekani na kujeruhu watu 100, na kuwaacha maelfu ya watu bila huduma ya umeme.

Vimbunga hivyo vimesababisha uharibifu mkubwa katika mji wa Sulphur, ulio na idadi ya watu takriban 5,000 ambapo vimesababisha kuporomoka kwa majengo, kupindua magari na kubomoa paa za nyumba. 

DW imeripoti kuwa, Katika ziara iliyofanywa na Gavana wa Jimbo hilo la Oklahoma, Kevin Stitt, amesema kwa jinsi inavyoonekana kia biashara mjini humo imeharibiwa na vimbunga hivyo.

Maafisa wa ikulu ya White House, wamesema kuwa Rais wa nchi hiyo Joe Biden amezungumza na Stitt na kutoa msaada kamili wa serikali hiyo ya shirikisho.