Mwenge wa Uhuru watua Mkoa wa Pwani, kuzindua miradi 126

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 07:24 PM Apr 29 2024
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, akipokea Mwenge wa Uhuru.
Picha: Julieth Mkireri
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, akipokea Mwenge wa Uhuru.

MWENGE wa Uhuru 2024 umepokelewa leo katika Mkoa wa Pwani ukitokea Mkoa wa Morogoro.

Akipokea Mwenge huo wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema utakimbikimbizwa km 1,225.3 ambapo utakagua, utazindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi 126 yenyewe thamani ya zaiidi ya sh trillion nane. 

Makabidhiano hayo ambayo yamefanyika katika eneo la Bwawani kata ya Ubena Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, yamehushuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani akiwemo mke wa Rais Mstaafu awamu ya nne Mama Salma Kikwete.

Akizungumza katika mapokeai ya Mwenge wa Uhuru  Kunenge amesema thamani ya miradi ya mwaka huu ni zaidi ya miradi ya mwaka  2023 ambayo ilikuwa na thamani ya sh. Trillion 4.4.

Amesema miradi 18 itawekwa mawe ya Msingi, 22 itakaguliwa na 16 itazinduliwa na kwamba Mafanikio ya uwepo wa miradi hiyo yametokana na uwekezaji na fedha zilizotolewa na Serikali.

Kunenge amesema Mkoa huo katika adhma yake ya kutunza mazingira umelenga kupanda miti miln 13.5 hadi kufikia mwezi June 2024 katika kipindi cha mwaka 2013/2024 na hadi sasa miti Miln 8,884,935 imepandwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, amesema utakimbizwa katika Halmashauri mbili Chalinze na Bagamoyo na miradi miradi 29 yenyewe thamani ya sh. Biln 15.2 itapitiwa.

Katika Halmashauri ya Chalinze kati ya miradi iliyopitiwa na Mwenge ni pamoja na  daraja Kijiji Cha Visakazi kata ya Ubena namna ulivyoakiso matumizi sahibi ya rasilinali fedha za umma na Wahisani.

Miradi mingine ni tanki la maji Mtambani ambao umejengwa kwa gharama ya zaidi ya sh.miln 160 katika  kata ya Bwilingu,shule ya Msingi Chalinze na kutembelea kikundi cha Vijana kata ya Pera na mradi wa Huduma ya kijamii.