Nyota wanaowania Kiatu cha Dhahabu Ulaya 2023-24

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:45 AM Apr 29 2024
news
Picha: Maktaba
Nahodha wa Timu ya Taifa ya England, na mchezaji wa Bayern Munich, Harry Kane.

KUFUNGA mabao ni biashara kubwa, haswa linapokuja suala la kusherehekewa kama mfungaji bora zaidi barani Ulaya. Kiatu cha Dhahabu ni tuzo iliyotengwa kwa moja tu kati ya tuzo zingine zote za Kiatu cha Dhahabu katika mashindano tofauti ya Klabu hususan ya Ulaya.

Huku msimu ukielekea mwisho, vinara wakuu barani Ulaya wamejipanga kupigana ili kupata tuzo ya mwisho kwa kuwa mfungaji bora zaidi barani humo.

Taji la Robert Lewandowski lilinyakuliwa na Erling Haaland msimu uliopita, huku raia huyo wa Norway akifunga mabao 36 katika mechi 72 na kuisaidia Manchester City kutwaa mataji matatu. Wachezaji kama Harry Kane (30), Kylian Mbappe (29), Alexandre Lacazete (27) na Victor Osimhen (26) walifuata katika tano bora.

Goal inafuatilia maendeleo ya wachezaji ambao wanawania kutwaa tuzo hiyo msimu wa 2023-24.

Kumbuka: Orodha inajumuisha wafungaji bora pekee kutoka Ligi Kuu England, LaLiga, Bundesliga, Serie A na Ligue 1.

 1. Harry Kane | Bayern Munich | Mabao 35

Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya England amewaondolea shaka mashabiki wake kwa kutumia kiwango chake cha ajabu nchini Ujerumani. Harry Kane tayari atakuwa wa pili baada ya Robert Lewandowski - ambaye alichukua nafasi yake huko Bayern – kufukuzia rekodi ya Gerd Muller ya mabao 40 kwa msimu huko Bundesliga.

 2. Kylian Mbappe | PSG | mabao 26

Mfaransa huyo amefunga wastani wa mabao 24 tangu kuhama kwake kutoka Monaco mwaka wa 2017. Akiwa amepungukiwa na bao moja kati ya 30 kwenye Ligue 1 msimu uliopita, fowadi huyo wa PSG, Kylian Mbappe, anaweza kumpiku Haaland huku wawili hao wakiwinda tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya msimu huu.

 3. Serhou Guirassy | Stuttgart | Mabao 25

Huenda lisiwe jina ambalo liko kwenye midomo ya kila mtu hivi sasa, lakini Sehrou Guirassy ameuchukua mchezo wa Ligi Kuu Ujerumani kwa kishindo tangu alipowasili kwa mkopo kutoka Rennes ya Ufaransa msimu uliopita. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Guinea amekuwa na wakati mzuri zaidi na mabao yake 25 hadi sasa.

 4. Lois Openda | RB Leipzig | Mabao 24

RB Leipzig wanajulikana kutengeneza washambuliaji wa kiwango cha juu duniani na haitashangaza iwapo Lois Openda atavutia ofa za juu, huku Mbelgiji huyo akifanya vema kwenye Bundesliga baada ya kukamilisha uhamisho wake wa majira ya joto kutoka Lens.

 5. Lautaro Martinez | Inter | Mabao 23

Mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina anaonekana kuwa mfungaji mkuu wa Nerazzurri na ana nia ya kuongeza mabao. Haijalishi Inter ilishindwa kumpata Romelu Lukaku.

 6. Cole Palmer | Chelsea | Mabao 20

Pengine usajili wa kushangaza zaidi katika kipindi cha majira ya joto kwa Chelsea ulikuwa ni kuwasili kwa kipa mwenye umri wa miaka 21 wa Manchester City, Cole Palmer, ambaye ameibuka kuwa mchezaji muhimu katika mfumo wa ushambuliaji wa 'The Blues' katika muda wake mfupi katika klabu hiyo. Siku zote akitafuta kuchunguza na kutengeneza mabao, uchezaji wake wa hali ya juu hadi sasa umevutia hisia za mashabiki.

 7. Erling Haaland | Manchester City | Mabao 20

Jina la Erling Haaland halipaswi kamwe kukushangaza kwa mtu anayetengeneza namba za wazimu mbele ya goli. Manchester City walijua walichokuwa wakipata msimu uliopita na raia huyo wa Norway anaendelea kutimiza matarajio, akifunga bao katika takriban kila mchezo huku akipania kutwaa Kiatu cha Dhahabu mfululizo cha Ligi Kuu England.

 8. Ollie Watkins | Aston Villa | Mabao 19

Ollie Watkins amekuwa akiivutia mara kwa mara katika misimu mitatu iliyopita. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa England amekuwa mtu muhimu katika ufufuo wa Villa chini ya Unai Emery na amekuwa akifichuliwa tangu Mhispania huyo alipomrithi Steven Gerrard Oktoba mwaka jana.

 9. Artem Dovbyk | Girona | Mabao 19

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ukraine, Artem Dovbyk, alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Girona msimu wa majira ya joto kutokana na msimu mzuri na Dnipro-1 ambapo alifunga mabao 32 katika mechi 48 kwenye mashindano yote. Tayari amethibitika kuwa mchezaji mahiri kwa Girona. Alifunga mabao 15 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, huku juhudi zake zikisaidia kikosi cha Unai Emery kufuzu kwa Ligi ya Europa.

 10. Alexander Isak | Newcastle | Mabao 19

Majeraha ndio kitu pekee kinachomzuia Alexander Isak kufikia uwezo wake, kwani ilishuhudiwa katika kiwango cha Msweden huyo kutokana na Kombe la Dunia la 2022 msimu uliopita ambapo alifunga mabao nane katika michezo 19 tangu Januari.

 11. Deniz Undav | Stuttgart | Mabao 18

Deniz Undav, ambaye alijiunga na Stuttgart kwa mkataba wa mkopo msimu uliopita, alistahimili kampeni mbaya msimu uliopita huku akifunga mabao nane pekee katika michezo 30 katika mashindano yote. Hata hivyo, anaonekana kuwa chanya kwenye Bundesliga, na anaonekana kuvuka lengo lake la msimu uliopita.

 12. Dominic Solanke | Bournemouth | Mabao 17

Dominic Solanke aliandikisha mchango mzuri wa mabao 13 katika Ligi Kuu msimu uliopita, akionekana kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi wa Bournemouth. Msimu huu, amepiga hatua zaidi.

 13. Mohamed Salah | Liverpool | Mabao 17

Akiwa na mabao 17 kwa jina lake, Mohamed Salah ndiye aliyekuwa kivutio kwa Liverpool licha ya matokeo mabaya ya Wekundu hao. Mmisri huyo kwa mara nyingine tena atatarajiwa kukiinua kikosi cha Jurgen Klopp kwa kiwango kikubwa zaidi.

 14. Jude Bellingham | Real Madrid | Mabao 17

Jude Bellingham amekaribia kusawazisha katika mpango wa Carlo Ancelotti huko Real Madrid msimu huu. Akifananishwa na Zinedine Zidane na kufikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kufunga mabao 10 katika mechi 10 za mwanzo alizocheza katika klabu hiyo.

 15. Jonathan David | Lile | Mabao 17

Jonathan David amekuwa katika kiwango cha kupachika mabao kwa Lille katika misimu michache iliyopita, na mchezaji huyo wa Kimataifa wa Canada anaonekana kuwa miongoni mwa matarajio ya kusisimua zaidi barani Ulaya kwa sasa.

 16. Ante Budimir | Osasuna | Mabao 16

Mkongwe wa Croatia, Ante Budimir alikuwa shujaa wa Osasuna katika fainali ya msimu uliopita, kwani mabao yake yaliisaidia timu hiyo ya Navarra kutinga hatua ya UEFA Europa Conference League kwa msimu wa 2023-24. Alimaliza msimu wa 2022-23 akiwa na mabao nane katika mechi 31, na tayari yuko njiani kuboresha idadi hiyo msimu huu.

 17. Dusan Vlahovic | Juventus | Mabao 16

Msimu uliopita wa majira ya joto, Juventus ilijaribu kubadilisha huduma za Dusan Vlahovic na nyota wa Chelsea, Romelu Lukaku. Mwishowe, hatua hiyo iliporomoka na Mserbia huyo akaishia kubaki pale kwenye dimba la Allianz, huku Mbelgiji huyo akijiunga na Roma kwa mkopo.

Ingawa mchezaji huyo wa zamani wa Fiorentina hajawahi kuwa kwenye kiwango bora kwa kiasi kikubwa kutokana na matokeo yake tangu alipohamia Juventus msimu wa baridi wa 2022, kwa mara nyingine tena anajiimarisha kama mchezaji wa kutegemewa katika soka la Italia, na ameanza vema kwa msimu wa sasa.

 18. Jarrod Bowen | West Ham | Mabao 16

Tangu kuondoka kwa Declan Rice, Jarrod Bowen amekuwa akiwaongoza 'Wagonga Nyundo' wa Landon kama mfungajina mtayarishaji wa mabao.

 19. Borja Mayoral | Getafe | Mabao 15

Borja Mayoral ameibuka kama msaada kwa Getafe tangu mapumziko ya Kombe la Dunia. Ufungaji wake wa mabao umesaidia hata timu hiyo ya Hispania kujiondoa kwenye eneo la hatari la kushuka daraja.

 20. Son Heung-min | Tottenham | Mabao 15

Kuvaa viatu vya Kane si jukumu dogo, lakini Son Heung-min anaendelea kupambana na hali yake katika kiwango cha kuongoza mashambulizi huku pia akiwa nahodha wa Tottenham.

 21. Ermedin Demirovic | Augsburg | Mabao 15

Nahodha wa Augsburg, Ermedin Demirovic ameendelea kuonesha kiwango kizuri kwa upande wake. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Bosnia alichangia mabao nane na asisti sita katika mechi 30 za Bundesliga msimu uliopita. 

 22. Alexandre Lacazette | Lyon | Mabao 15

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Alexandre Lacazette, amefanya vema tangu arejee kwenye Ligue 1, na aliisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi msimu uliopita kutokana na kiwango chake kizuri cha upachikaji mabao. Ingawa hajafanya vema katika kampeni hii, 'Les Gones' wanahitaji nahodha wao kuwa fiti na kufyatua mipira yote, huku Lyon wakiwa katika matatizo makubwa ya kushuka daraja.