Kishindo uzinduzi wa maandalizi ya mbio za Great Ruaha Marathon 2024

By Francis Godwin , Nipashe
Published at 03:56 PM Apr 28 2024
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Great Ruaha Marathon walioshiriki Uzinduzi wa Vifaa vya kukimbilia (KIT)Jana
Picha: Francis Godwin
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Great Ruaha Marathon walioshiriki Uzinduzi wa Vifaa vya kukimbilia (KIT)Jana

MAANDALIZI makubwa yameanza kufanyika kwa ajili ya msimu wa tatu wa mbio za mwendo pole na haraka za Great Ruaha Marathon (GRUMA) 2024 zitakazofanyika Julai 6, mwaka huu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.

Katika Uzinduzi wa Vifaa vya kukimbilia (KIT)ulioambatana na Filamu fupi yenye maudhui ya kabila la kihehe uliofanyika hotel UNUNIO BEACH PARK Jijini Dar es Salaam Jana  umeonesha jinsi ambayo Maandalizi hayo yalivyo na mvuto mkubwa zaidi .

Baadhi ya washiriki walioshiriki kwenye Uzinduzi huo akiwemo Sarah John walisema wamevutiwa zaidi kwenda mkoani Iringa kushiriki Mbio hizo zitakszo shirikisha wakimbiaji toka  sehemu mbalimbali Duniani .

  Mbio hizo zinazoandaliwa na Taasisi ya Sustainable Youth Development Partnership Tanzania (SYDP) kupitia mratibu wake mkuu  Amim Kilahama alisema kuwa Maandalizi yameandaliwa kwa kiwango Cha juu zaidi ili kuvutia zaidi washiriki na kuona tofauti ya Mbio nyingine.

Maandalizi ya mbio hizo zinazolenga kuhamasisha utalii wa kusini, kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuhamasisha jamii ya kitanzania kushiriki michezo ili kulinda afya zao, yalizinduliwa jana kwa kuonesha medali zitakazotolewa kwa washindi na vifaa rasmi vitakavyotumika kukimbilia.

Alisema kutakuwa na Mbio za  kilometa tano, 10 na 25  uzinduzi huo.

Kilahama amewaomba wadau wa utalii na uhifadhi ikiwemo wizara husika, Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji, na wawekezaji wa sekta hiyo kujitokeza kudhamini mbio hizo zinazotarajia kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 1,000 .

“Kama mtakumbuka mwaka jana tulikuwa na washiriki zaidi ya 200 wakiwemo waliotoka Ujerumani, Japan, China na Australia; mwaka huu tunatarajia kupata washiriki wengi zaidi kutoka mataifa ya kigeni,” alisema.

Toka wameanza huu ni msimu wa tatu wadhamini wamekuwa Mabata Makali Lodge and Campsite,Ununio Beach park na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha .

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambao ni waratibu wenza wa mbio hizo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Godwell Ole Meing’ataki amesema wanaitumia GRUMA kuthibitisha namna inavyochochea uhifadhi na kukuza utalii kwa kuvutia washiriki na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali.

“Mbio hizi zimekuwa zikivutia watu kusafiri kuja hifadhini na kushiriki, kushuhudia na kufanya utalii, hivyo kuchochea utalii na kuleta faida kwa nchi na jamii inayozunguka hifadhi hii ya pili kwa ukubwa nchini,” 

Alitoa wito kwa mashirika na wadau mbalimbali wa utalii kujitokeza kuongeza nguvu ya udhamini wa Mbio hizo.