NDANI YA NIPASHE JUMAPILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa mchezaji wa klabu ya Simba Clatous Chama alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi. (Picha kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa kocha wa klabu ya Simba Pablo Franco alietangazwa kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wapili kushoto), akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa moja ya makampuni yaliyoshinda tuzo za Usalama na Afya mahali pa kazi na OSHA ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani Aprili 22, 2022.