Burkina Faso yafungia mashirika saba ya habari ya kimataifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:47 AM Apr 29 2024
Studio ya habari.
Picha: Anthony Anex/picture alliance/KEYSTONE
Studio ya habari.

SERIKALI ya Burkina Faso, imesimamisha matangazo ya mashirika kadhaa ya habari baada ya kuiangazia ripoti ya shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch (HRW) iliyodai kuwa jeshi la nchi hiyo linatekeleza mauaji ya kiholela.

Miongoni mwa mashirika yaliotajwa katika agizo hilo ni gazeti la Ufaransa Le Monde, gazeti la Uingereza The Guardian, Deutsche Welle ya Ujerumani na Kituo cha televisheni cha Ufaransa TV5 Monde. 

Vyombo vingine vya habari vilivyotajwa katika agizo hilo ni gazeti la kikanda la Ufaransa la Ouest-France, APAnews na Agence Ecofin.

Siku ya Alhamisi CSC ilitangaza kuwa imeagiza kampuni za huduma za mtandao wa intaneti kukata huduma zake kwa wiki mbili kwa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC na lile la Marekani la Voice of America VOA, kwa kuiangazia ripoti hiyo ya HRW.