Mashambulizi ya anga Syria yaua zaidi ya watu 10

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:20 PM Mar 27 2024
Jengo lililoharibiwa na shambulizi la anga katika mji wa kusini mwa Syria wa Deir Ezzor, Machi 26, 2024.
Picha kwa hisani ya AFP
Jengo lililoharibiwa na shambulizi la anga katika mji wa kusini mwa Syria wa Deir Ezzor, Machi 26, 2024.

MFULULIZO wa mashambulizi ya anga mashariki mwa Syria yameua zaidi ya watu 10, akiwemo Mshauri wa Jeshi la Iran na mfanyakazi wa shirika la afya duniani (WHO), maafisa na ripoti zimesema.

VOA imeripoti kuwa, Haikufamika wazi mara moja nani alihusika na mashambulizi hayo ya anga katika mkoa wa mashariki mwa Syria wa Deir el-Zour ambao unapakana na Iraq.

Shirika linalofuatilia haki za binadamu lenye makao yake Uingereza, lilisema mashambulizi hayo yaliua watu 15, akiwemo mshauri wa kikosi cha mapinduzi cha Iran, walinzi wake wawili, pamoja na wapiganaji tisa wa Iraq wa kundi linaloungwa mkono na Iran na raia wawili wa Syria wanaofanya kazi na Wairan.

Shirika la habari la serikali ya Iran limethibitisha kwamba mwanachama wa kikosi cha mapinduzi aliuawa nchini Syria.

WHO imesema mmoja wa wafanyakazi wake, muhandisi Emad Shebab aliuawa katika moja ya mashambulizi dhidi ya jengo lake.