ACT Wazalendo yaja na vipaumbele 10 Uchaguzi Serikali za Mitaa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:36 PM Mar 28 2024
Naibu Katibu Mwenezi, ACT Wazalendo, Shangwe Ayo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Naibu Katibu Mwenezi, ACT Wazalendo, Shangwe Ayo.

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Naibu Katibu Mwenezi wake Shangwe Ayo kiimesema serikali inapaswa kupeleka Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Bunge lijalo na kusisitiza maeneo 10 ambayo yanahusu ushirikishwaji, uwazi na uadilifu kwenye mchakato wa uchaguzi huo.

Shangwe ametaja maeneo hayo leo Machi 28, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari, na hapa Nipashe Digital inakuwekea maeneo manne tu kati ya 10. Kesho Machi 29, katika Gazeti lako la Nipashe utasoma habari hii kwa undani zaidi.... 

1/DAFTARI LA WAPIGAKURA LIWE MOJA

"Kwa vile Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi imeipa madaraka Tume kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo tunapendekeza daftari la wapigakura liwe moja. Daftari linalotumika Uchaguzi Mkuu litumike pia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa" 

2/USIRI UZALISHAJI KARATASI ZA KURA IWE MWISHO

"Tuanataka wadau, hasa vyama vya siasa, tushirikishwe kwenye uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa karatasi za kura ili kudhibiti vitendo viovu vya kuwapa kura makada wa CCM"

3/MAWAKALA WA VYAMA WASILE KIAPO

"Kwa vile mawakala wanawakilisha maslahi ya wagombea na vyama vyao, utaratibu wa sasa wa kula kiapo usitishwe. Wagombea na vyama wawe na uhuru wa kupendekeza, kutambulisha na kubadili mawakala" 

4/KAMPENI SI CHINI YA WIKI MBILI

"Uchaguzi uliopita wa Serikali za Mitaa, Kampeni ilikuwa Wiki Moja. Awamu hii, ACT Wazalendo tunapendekeza kampeni isipungue wiki mbili kuwapa wagombea nafasi ya kujinadi vizuri"-