Umoja wa Makatibu wakuu wastaafu waliowahi kuhudumu Wizara mbalimbali nchini wamelipongeza Shirika la Reli Tanzania TRC kwa kuanzishwa kwa Reli ya Kisasa ya SGR kwani kutaweza kuwasaidia Usafirishaji wa Mizigo na Abiria kwa Haraka zaidi na kuondokana na Changamoto ya Usafirishaji nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu Wakuu Wastaafu nchini Michael Mwenda wakati wa Ziara ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa kutembelea reli ya Kisasa ambapo Umoja wa Makatibu Wakuu Wastaafu waliambana na Bodi ya Wakurugenzi sambamba na Wafanyakazi wa TRC.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk. Ali Possi amewatoa hofu Makatibu Wakuu Wastaafu waliowahi kuhudumu Wizara mbalimbali nchini kwani bado wanaendelea kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali sambamba na kuendelea kukutana kuongeza uzoefu na maarifa zaidi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TRC, Amina Lumuli, amesema kuwa kipande cha SGR Dodoma kimefika zaidi ya asilimia 96 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuanza majaribio kutoka Dar es Salaam - Dodoma.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED