Rais Samia ampongeza Diomaye kwa kushinda urais Senegal

By Dotto Charles , Nipashe
Published at 04:36 PM Mar 27 2024
Rais Samia Suluhu Hassan.
PICHA: IKULU
Rais Samia Suluhu Hassan.

RAIS Samia Suluhu Hassan, amempongeza Bassirou Diomaye Faye kwa kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Jamhuri ya Senegal.

Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram, huku akisema kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Senegal

“Nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Senegal, Bassirou Diomaye Faye, kwa ushindi ulioupata katika uchaguzi wa urais wa 2024 wa Senegal; na ninawapongeza watu wa Senegal kwa uchaguzi huo wa amani. Na ninatarajia kufanya naye kazi tukiimarisha uhusiano kati ya nchi zetu.”