Manara atambulishwa balozi mpya Parimatch

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:47 PM Apr 15 2024
Balozi wa Parimatch, Haji Manara (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Erick Gerald (kulia) na Meneja wa Masoko, Levis Paul katika hafla ya kumtambulisha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Balozi wa Parimatch, Haji Manara (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Erick Gerald (kulia) na Meneja wa Masoko, Levis Paul katika hafla ya kumtambulisha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Parimatch Tanzania imemtambulisha rasmi Haji Sunday Manara ‘El Bugati’ kuwa balozi wao mpya.

Ujio wa Manara umeelezewa kuwa mzuri kwa kampuni hiyo yenye ofa za kijanja na tovuti ambayo inamuonekano mzuri na kasi kubwa ya intaneti.

Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu Masoko wa Parimatch, Levis Paul, amesema Manara atawasaidia sana kuitangaza na wateja wao kuweza kushea mikeka yao kwa marafiki ili nao waweze kupata burudani ya kampuni hiyo.

“Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Haji Sunday Manara kama balozi wetu kwa ajili ya kuzidi kupata burudani. Yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza kwa upande wake kulizungumzia vema soka la Tanzania bila ya kusahau kuwapa thamani wachezaji wetu wa ndani na wa kimataifa pindi wanapocheza katika ardhi yetu”, amesema Paul.

“Kupitia balozi wetu tuna hakika ataipeperusha vema Chapa ya Parimatch kila eneo pamoja na kusaidia kutoa uelewa kwa wachezaji maana halisi ya kubeti ili wote tuweze kufurahi na kucheza kistaarabu.” 

Kwa upande wa Manara, amesema: “Kiukweli nilipigiwa simu na kampuni nyingi, lakini katika uchunguzi wangu nikabaini kuwa Parimatch ndio kampuni bora kwangu kufanya nayo kazi kwa sababu inaaminika duniani kote na katika hili nyinyi mtakuwa mashahidi wa hili. 

“Msimu uliopita walikuwa wameidhamini Klabu ya Mbeya City iliyokuwa inashiriki ligi yetu pendwa ya Tanzania na kwa msimu huu klabu mbili zinadhaminiwa na kampuni hii.

 “Ukiachilia mbali masuala ya soka, hawa Parimatch pia wanathamini sana vipaji vya muziki na vichekesho vya vijana wetu na ndio sababu mnawaona hapa hawa vijana wenzangu tupo pamoja hapa. Mbali na hilo hii ndio kampuni kinara kwa michezo ya kubashiri mtandaoni na inapatikana katika zaidi ya nchi 15 duniani na ikiwa na wateja zaidi ya milioni. 

“Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha nanyi ndugu zangu wapenda michezo ya soka kuja kujiunga na familia kubwa ya Parimatch kwani ukiwa huku utafurahi kwa malipo ya papo hapo, 'Odds' kubwa na masoko ya kila aina, yaani ushindwe wewe tu.”

“Kwa kumalizia niwakumbushe Watanzania pamoja na wadau wote wa kubeti kuwa Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!” ameongeza kusema.