Rais Samia ateua, atengua, Prof. Ndalichako aachwa, Makonda Arusha

By Frank Monyo , Nipashe Jumapili
Published at 10:51 AM Mar 31 2024
Picha ya kuunganishwa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),Profesa Joyce Ndalichako (kushoto)  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda.
Picha: Maktaba/Nipashe Digital.
Picha ya kuunganishwa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda.

Leo Jumapili, Machi 31, 2024 Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na utenguzi na kuhamisha viongozi mbalimbali katika nafasi zao.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho, uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa  na wilaya.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, akichukua nafasi ya John Mongella ambaye atapanagiwa kazi nyingine.

Makonda aliyedumu katika nafasi hiyo ya Uenezi wa CCM kwa takribani miezi mitano, aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia katika mabadiliko hayo yamemweka pembeni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),Profesa Joyce Ndalichako katika baraza la mawaziri huku nafasi yake ikichukuliwa na Deogratius Ndejembi ambaye ameteuliwa kuchukua mikoba yake. Ndjembi alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.