DEREVA HONELO RAMADHANI...Kutoka enzi teksi yake ya wateja kijiweni, hadi ufanisi mtandaoni

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:22 AM Mar 29 2024
news
Picha: Mpigapicha Wetu.
Dereva Honelo Alli Ramadhani.

AKIWA na uzoefu wa takribani miaka tisa katika tasnia ya usafiri wa kukodi mtandaoni nchini, Honelo Alli Ramadhani, ana mengi ya kueleza kuhusu tasnia ya uchukuzi wa kidijitali, ambayo ameuona ukikua kutoka miaka ya nyuma hadi sasa.

Huyo baba wa watoto watatu mwenye umri miaka 41, akianzia udereva wa teksi za kawaida. Ameanza kufanya shughuli za kubeba abiria nchini, mwaka 2015. Kwa sasa, anafanya kazi kwenye mtandao wa Bolt Tanzania kama dereva wa gari la kifahari.

Kukodi usafiri mtandaoni, wakati mwingine hujulikana kama ‘kukodi gari kwa simu janja’.Ni njia ya usafiri binafsi, ambao abiria humtumia dereva kupitia programu ya simu mkononi kumpeleka mahali halisi.

Ulikuwa wakati wa ujio wa teknolojia hiyo, Honelo alipofikiria kujiunga na kikundi cha madereva, kwani teksi za kawaida zilipotea na abiria wengi kibinafsi walichagua huduma mpya za bei nafuu na uhakika.

Akiwa miongoni mwa madereva wa kwanza kutumia njia mpya ya usafiri binafsi, Honelo akakumbuka jinsi madereva wengi wa magari walipata shida kuendesha mfumo kupitia programu za simu za mkononi.

 "Wakati huo, wengi wetu hatukuweza kusoma ramani kama inavyoonyeshwa kwenye simu janja, ili kupata abiria wanaotarajiwa na wakati mwingine, mtandao unaweza kukumbwa na hitilafu ambayo ilisababisha hasara ya mapato," Honelo anaeleza alipohojiwa na gazeti  hili.

Hata hivyo, sasa anafuraha programu imeboreshwa, hata kukiwapo hitilafu yoyote, madereva huarifiwa mara moja. Anafafanua: “ikitokea kuharibika kwa mtandao wowote, madereva wanajulishwa na mara nyingi kesi kama hizo hutatuliwa ndani ya muda mfupi sana."

Akizungumzia anavyopata kipato zaidi, mjini Dar es Salaam, kunakosifika kwa kero ya msongamano wa magari, Honela anasema huwa anashauriana na abiria, wakatumia njia za kuunganisha tofauti na barabara kuu.

 "Kama dereva wa gari, ni muhimu kushauriana na abiria wako ikiwa unaweza kutumia njia za kuunganisha, ili kuepuka msongamano wa magari katika barabara kuu. Hii huniwezesha kuepuka kuchukua muda mrefu kwenye njia moja na hatimaye kuniwezesha kupata pesa zaidi.

"Pia, ninawauliza kama wanapenda kusikiliza muziki au taarifa za habari kama njia ya kuwafanya wastarehe. Mwanzoni pia, haikuwa rahisi kuwasiliana na abiria wa kigeni kutokana na kikwazo cha lugha, lakini kwa miaka mingi nimejifunza mengi na angalau naweza kuwashirikisha katika mazungumzo madogo,” anaieleza.

Honela anatamka kufurahi maisha yake kubadilika tangu kuijikita katika udereva mtandao wa Bolt Tanzania, akiwa katika kiwango cha juu amejipatia gari lake, kupitia mkopo kwake kutoka taasisi ya fedha.

"Sidhani kama ningekuwa katika nafasi ya kununua gari kama dereva wa teksi, lakini shukrani kwa kampuni ya Bolt Tanzania sasa nina miliki gari langu nililolipata kwa njia ya usafiri mtandaoni," anashukuru.

 MATATIZO YALIYOKO

Kama ilivyo biashara nyingine, usafiri wa abiria una matatizo yake kama vile abiria wakorofi na walevi, wanaokataa kulipa kiasi kinachohitajika, wanapofika  mwisho wa safari zao.

"Lazima utumie hekima unaposhughulika na watu kama hao. Iwapo abiria atakataa kulipa kiasi kinachohitajika, basi nitaripoti kesi kama hiyo kwa Bolt Tanzania, ambao watanirudishia baada ya muda,” anaeleza.

Kuhusu usalama unapoendesha gari kwa watu usiowajua, Honelo anasema hana wasiwasi kwa kuwa programu za kuwapokea abiria kwa Bolt hutoa taarifa zote za abiria, kama mahali anakotoka.

"Ukiwa kama dereva, unazungumza na abiria wako kabla hata ya kukutana nao na habari zote na njia zinajulikana kupitia App," anafafanua.

Ili kukabiliana na mahitaji mapya ya abiria, Bolt Tanzania inatuma barua pepe kwa madereva wote kuhusu bidhaa na huduma zote mpya, kama vile ofa za wateja na nyenzo za usalama kwenye App zao.

Anasema, hilo limewafanya madereva waendesha magari, kuwa sawa na maendeleo mapya katika kampuni yake, sasa akitabiri mustakabali mzuri wa huduma za Taxi Mtandao nchini, kwa kuwa abiria wengi wanataka huduma za bei nafuu na za kutegemewa kama zile zinazotolewa na Bolt Tanzania.

“Bolt Tanzania imefanya kazi kubwa ya kutuunganisha na wateja wanaotaka bei nafuu. Ilikuwa ngumu sana kwetu nyakati za zamani, lakini mambo yamerahisishwa kupitia matumizi ya teknolojia,” anakiri.

Anawashauri wengine wanaotaka kujiunga na udereva, wasisite kuingia katika tasnia hiyo, akijivuna ni ya uhakika na rahisi, ikiwezesha watu kujihusisha na shughuli nyingi.

Katika muda wa ziada asipokuwa kazini, Honelo anasema hutumia kuwa nyumbani akiwa na mke, pia watoto.

Ndoto za Honelo sasa, ananuia kununua kiwanja na kujenga nyumba, kisha akafungua biashara itakayomsaidia uzeeni katika umri hawezi tena kujishughulisha na uendeshaji gari.