Mtaka ataka vipaji kuendelezwa

By Elizabeth John ,, Adam Fungamwango , Nipashe
Published at 05:25 PM Apr 24 2024
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka akizungumza katika hafla ya kupokea mipira iliyotolewa na TFF.
Picha: Elizabeth John
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka akizungumza katika hafla ya kupokea mipira iliyotolewa na TFF.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema kuna kila sababu ya kuendelea kukuza vipaji vya watoto kupitia mpira wa miguu kwa sababu hivi ni biashara ambayo inazalisha mabilionea.

Mtaka ameeleza hayo mjini Njombe wakati akipokea mipira 1,000 iliyotolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kwa ajili ya shule za msingi.

Aidha Mtaka ameongeza kuwa, kwa sasa katika mapinduzi ya nne ya viwanda, dunia inashuhudia michezo ikizalisha mabilionea na matilionea.

"Kwenye mapinduzi ya nne viwanda karne ya 21, dunia inashuhudia michezo ikizalisha matajiri na mabilionea na football ikiwa ni mchezo mama unaoongoza kuzalisha ajira na wafanyabiashara wakubwa," amesema Mtaka.