Utulivu, busara wahitajika dirisha la usajili likikaribia
WAKATI msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa 2023/2024 ukitarajiwa kumalizika ifikapo Mei 28, mwaka huu, tayari klabu mbalimbali zimeshaanza mchakato wa kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya kuwatumia kwenye msimu mpya.