Jeshi la Ukraine lashambulia uwanja wa ndege Urusi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:48 AM Apr 18 2024
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema jeshi lake limeshambulia uwanja mkubwa wa ndege wa Urusi wa Dzhankoi katika eneo linalokaliwa la Crimea na kuwasifu makamanda wake walioongoza oparesheni hiyo.

Zelensky ametaja oparesheni hiyo kuwa ni yenye mafanikio kutokana na jeshi la Ukraine, kuripoti kuharibu miundombinu pamoja na vifaa vya kijeshi vya Urusi katika oparesheni hiyo iliofanyika kaskazini mwa rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na kukaliwa na Urusi mwaka 2014.

Kwa upande mwingine Urusi imeendelea kuvurumisha makombora katika miji ya Ukraine, ambapo makombora matatu yameanguka katika mji wa kihistoria wa Chernigiv na kuuwa watu 17.

Serikali ya Kyiv imeendelea kuomba mifumo ya ulinzi wa anga kutoka kwa washirika wake, ikiwemo Ulaya na Marekani.