Maporomoko ya udongo yaua watu 15 Kongo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:08 PM Apr 15 2024
Maeneo mengi ya milima nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hukumbwa na maporomoko ya udongo msimu wa mvua kubwa.
Picha: GLODY MURHABAZI/AFP
Maeneo mengi ya milima nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hukumbwa na maporomoko ya udongo msimu wa mvua kubwa.

MAPOROMOKO ya udongo kusini magharibi mwa Kongo, yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 15 huku wengine zaidi ya 60 wakiwa hawajulikani walipo.

Gavana wa mpito nchini humo, Félicien Kiway amewaambia waandishi habari kwamba timu ya waokoaji imetumwa katika Jimbo hilo kwaajili ya kujaribu kuwaokoa manusura.

Kando na taarifa hizo, Mbunge wa Jimbo la Idiofa, Dhedhe Mupasa amesema Jumamosi watu saba walipatikana wakiwa hai karibu na bandari ilioko katika jimbo hilo na kwa sasa wanapata matibabu hospitalini.

Afisa mmoja ametahadharisha kwamba itakuwa vigumu kujua idadi kamili ya watu waliopotea, kutokana na eneo hilo kutumiwa kama soko la wazi siku ya Jumamosi, huku akilielezea eneo hilo la tukio kama mahali pa ubadilishanaji wa biashara ambapo wavuvi wanalitumia sana kuuza samaki na kununua sabuni.

DW