Maporomoko ya udongo yaua watu 33 Afghanistan

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:36 PM Apr 15 2024
Athari za mvua kubwa zilizonyesha nchini Afghanistan.
Picha: SANAULLAH SEIAM/AFP/Getty
Athari za mvua kubwa zilizonyesha nchini Afghanistan.

ZAIDI ya watu 30 wamefariki kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyotokea nchini Afghanistan ikiwemo katika mji mkuu wa Kabul.

Msemaji wa utawala wa Taliban nchini humo, Abdullah Janan Saiq katika Wizara ya kushughulikia udhibiti wa majanga ya asili amesema wengi wa walioangamia waliangukiwa na nyumba zao baada ya mvua kubwa kunyesha.

Saiq amesema hadi sasa ni watu 33 waliofariki na wengine zaidi ya 27 wamejeruhiwa.

Maporomoko ya udongohayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa yaliyosababisha ubaribifu wa mali pamoja na vifo. Mvua hiyo inayotarajiwa kuendelea kunyesha imeziharibu zaidi ya nyumba 600, barabara pamoja na mashamba.