Majaliwa kufanya ziara Mlimba, maeneo yaliyokumbwa na mafuriko

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:10 PM Apr 15 2024
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya, akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya, akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Mlimba kujitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye anatarajia kufanya ziara kujionea maeneo yaliyoathirika na mvua.

Wito huo ametoa katika Mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Mlimba leo  Aprili 15,2024 ambapo amewaomba wananchi kujitokeza mapema  kwa wingi kesho.

"Waziri Mkuu atapata nafasi ya kuwapa pole wenzetu waliokumbwa na mafuriko ya mvua na tutapata wasaa wa kuwasilisha taarifa zetu" amesema Kyobya na kuongeza kuwa;

“Nishukuru Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kusaidia kuokoa watu kama mnavyofahamu kutokana na mafuriko ya hayo ya mvua, treni ya Udzungwa iliyokuwa na watu ilizuiwa kufika Mlimba lakini jeshi letu la Tanzania lilisaidia kuwaokoa watu na hakukutokea madhara yoyote”

Aidha serikali ilisaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua kupata chakula cha msaada ambacho kililetwa na helikopta.