Gavu: CCM haitashika dola kwa mabavu wala bunduki

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 09:01 PM Apr 16 2024
Katibu  wa NEC - Oganaizesheni Issa Haji Gavu.
Picha: Halfani Chusi
Katibu wa NEC - Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

Katibu wa NEC - Oganaizesheni Issa Haji Gavu , amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kamwe hakitashika dola kwa mabavu wala kutumia bunduki bali kwa njia za kidemokrasia.

Gavu ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa chama, Serikali, taaisisi ziziso za kiserikali, viongozi wa dini, wazee na machifu katika kikao cha ndani katika Kata ya Mlowo, wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe ikiwa ni mwendelezo wa ziara za chama hicho.

"Hatutashika dola kwa mabavu wala bunduki bali tutashika dola kwa njia za kidemokrasia. Msingi wa demokrasia ni kupiga kura, ili mwanadamu ashawishike basi una wajibu wa kumshawishi kabla ya kupiga kura", amesema na kuongeza;
"Tuhakikishe tunaendelea kuhamasisha na kuchapa kazi kwakuwa ndio kitu pekee kitakachoendelea kutupa thamani kwa wananchi kuendelea kutuamini"