Maporomoko ya tope yasababisha shule 5 kufungwa Mbeya

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:08 PM Apr 15 2024
Maporomoko ya tope yasababisha shule kufungwa Mbeya.
PICHA: MAKTABA
Maporomoko ya tope yasababisha shule kufungwa Mbeya.

TAKRIBAN shule tano jijini Mbeya zimefungwa kwa muda wa wiki moja kama tahadhari kutokana na maporomoko ya tope yaliyotokea jana katika eneo la Itezi, miongoni mwa shule hizo zilizofungwa ni pamoja na shule nne za msingi ambazi ni Generation, Mafanikio, Marys na Tambukareli na shule moja ya sekondari ambayo ni Itezi.

Kaimu Afisa Elimu wa Jiji la Mbeya Ally Omar Abdalah, amethibitisha kufungwa kwa shule hizo, ambapo amesema shule hizo zitawafanya wanafunzi zaidi ya 3,000 kukosa masomo kwa muda.

Abdalah amesema shule ya Tambukareli imefungwa kwa ajili ya kambi maalumu ya waathirika na shule ya Generation imefukiwa na tope zito kutoka mlima Kawetele.