Masauni aonya wanaotukana viongozi mitandaoni

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 08:43 PM Apr 15 2024
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, ameonya watu ambao wamekuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii kutukana viongozi wakuu wa serikali na kusisitiza hakuna mtu ambaye atafanya uhalifu asichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano, Masauni amesema serikali haitamfumbia macho mtu yeyote ambaye atabainika kuvunja sheria za nchi bila kujali cheo chake.

"Hakuna mtu yeyote ambaye atavunja sheria halafu serikali imuache tuu bila kumchukulia sheria kwani hakuna aliye juu ya sheria bila kujali nafasi yake,"amesema

Aidha, amewataka watanzania kuendelea kutii sheria na kuacha kujihusisha na mambo yanayovunja sheria za nchi kwenye mitandao ya kijamii.